Kabla ya kikao cha mambo fulani akijaanza watu tukaanza kupata Vimwetumwetu kwanza,simnaniona na kafulana kangu ka mistarimistari?
Hapo mambo fulani yameshaiva kila mmoja anaumiza kichwa kivyake babaa..Mnyamwezi nimetulia sikubali kushindwa jamani.
Hakuna kikao kinachokosa mapumziko,ilipofika mapumziko kila mtu akajiachia mtandao wake mezani na kwenda kuweka matumbo kitu chochote.
Watu kwa chai bwanaa..!! mie na chai wapi na wapi jamani?hata kama kuna baridi vipi chai hapa haipandi kabisaa.
Yani ninavyoipenda YANGA mpaka juisi nikinywa ni ya YANGA...aaaah nimekumbuka kumbe YANGA bingwa eeeh?Haya jamani kikao chetu kiliishia hapa nikawa nawapa jamaa story za YANGA,yani hata hawaijui kabisaa..kulia kwangu(kushoto kwako) ni jamaa yangu kutoka kule kwa kiongozi aliyeng'ang'ania madaraka mpaka akanyongwa kuleee Ira...na kushoto kwangu(kulia kwako)ni mdada niliyekutana nae kwenye huo mkutano kutoka pande zileeee za wachezaji wa mpira wa miguu alikotokea Roger Milla na Samu'el E'too.
0 Comments