Huyu mtu huyu anakusafishia nyumba yako nzima,anakupikia chakula cha familia yako yote,anakuoshoea vyombo vyako ulivyochafua na familia yako,anakufulieni nyote mpaka nguo zenu za ndani,ni mlinzi wa nyumba nyakati nyie mpo katika kutafuta riziki,anawaangalia watoto na kuaogesha na anapokea matusi na manyanyaso toka kwenu nyote,analala wa mwisho na kuamka wa kwanza.Na inapokuja suala zima la malipo yake kumzungusha ndio fasheni na humpi pesa zake zote.kwa kweli inasikitisha sana ukiangalia majukumu uliyompa na kipato chake hakilingani kabisaa,ukiulizwa nini?"unasema hakusoma"Hakusoma vipi...!!mbona ukimtuma magazeti anakuletea?mbona ukimtuma mahitaji mengine anakutimizia na hata ukimuelekeza dozi ya dawa ya mwanao anampa na kupona?Tuwajali sana hawa wasaidizi wetu kwa hali na mali.