Waumini wa kiislam nchini Tanzania wamefanya maombi maalumu kwa Taifa lao ili kumuomba MUNGU kuinusuru nchini na matatizo yanayolikabili nchi yao na bara la Afrika kwa ujumla.
Maombi hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Waislamu ya Taibah Tanzania kwa lengo la kuliombea Taifa lisiende pabaya kwa kugawa watanzania kwa matabaka.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Shehe Hassani Kiburwa, alisema wameamua kufanya Maulid hayo ya kuombea amani ya nchi, baada ya kuona kuna dalili za kutoweka kwa utulivu na amani nchini.

Katika maombi hayo waislamu walitoa wito kwa serikali kuwashughulikia wale wote wanaoonekana kutaka kulipeleka taifa pabaya

Waliitaka serikali kuwashughulikia watu hao wanaoonekana kutaka kuligawa taifa hili kwa ukabila, udini na hata wanaotaka kulifanya taifa hilo kama lao binafsi na kusahau wananchi

“Nchi hii ni ya wote na waliomo pia wanatoka kumoja, Watanzania sote tunasafiri katika jahazi moja, hivyo kama kuna mmoja