KUTOKANA na kero na uharibifu unaosababishwa na kunguru weusi nchini zaidi ya billion 1 imetengwa kuteketeza kunguru hao katika mradi utakaofanyika katika kipindi cha miaka miwili.Mbinu mpya za kupambana na kuwamaliza kunguru hao imeandaliwa na imedaiwa hadi ifikapo mwaka 2013 kunguru hao wasionekane kabisa nchini.

Hii imekuja baada ya kuonekana kunguru hao kuchangia kupoteza kasia jamii ya ndege na viumbe vingine wadogowadogo waishio maeneo ya Pwani.

Hayo yalijulikana hivi karibuni baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira Tanzania (WCST), Bi. Anne Lema alipiokuwa akitoa taarifa kuhusiana na mradi huo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema, msaada kutoka balozi za Dernmark, Finland na Shirila la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) ambao kwa pamoja wamechangia Dola za Marekani 748,200 sawa na Sh bilioni 1.12 kufanikisha mradi huo kwa muda wa miaka miwili.

Mbali na hao pia Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Idara ya Wanyamapori imetoa kiasi cha Shilingi milioni 150 ambazo zimetumika kuendesha shughuli za awali za mradi huo.

Amesema mikakati iliyowekwa na serikali kwa kushirikana na wadau hao watateketeza ndege hao kwa kutumia sumu, risasi na mitego mingine kuwaangamiza kunguru hao.(source Nifahamishe)