Waandamanaji nchini Syria wameripoti kuwa watu 60 wameuliwa na majeshi ya usalama- idadi kubwa kutokea katika kipindi cha wiki tano cha ghasia dhidi ya Rais Bashar al-Assad.
Waandamanaji hao walipigwa risasi walipokusanyika kwa ajili ya sala ya Ijumaa, siku moja baada ya amri ya hali ya hatari iliyodumu kwa miongo mingi kuondolewa.
Imeripotiwa vifo vingi vilitokea katika kijiji kimoja karibu na Deraa upande wa kusini, na kwenye kitongoji kwenye mji mkuu, Damascus.

Inasemekana takriban watu 260 wamefariki dunia tangu ghasia kuanza nchini humo mwezi uliopita.
Picha za video zilizotolewa zimeonyesha mapambano huku ufaytuaji risasi ukitumika.
Kuondoa amri ya hatari kulionekana kama jambo ambalo lingewaridhisha waandamanaji.
Katika taarifa yao ya pamoja tangu maandamano yalipoanza , wanaharakati walioandaa maandamano wametaka kuundwa kwa mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia.
Vurugu za kisiasa Syria zilianza baada ya maandamano kuzuka katika maeneo mengine ya nchi za kiarabu, ambapo kumeshuhudiwa kung'oka kwa marais wa Tunisia na Misri na kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe Libya.(sourse-bbc)