Idara husika katika miundombinu mabosi maofisini suruali hazifungi kwa jinsi matumbo ya rushwa na kula pesa za wananchi wanaolipa kodi kila mwezi,ila angalia mvua zinaponyesha barabara zilizolipiwa kodi na wananchi hao zinakuwajae???? Viongozi wa Afrika hawazinduki mpaka watolewe kwa kashfa au watu wafanye vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuuana au wakamatwe na umoja wa mataifa na kufungwa au kunyongwa ndipo wanajua kuwa kung'ang'ania madaraka sio kuzuri,jamani msinifikirie vibaya,sichochei wala siombei vita nchini kwangu,hali ya maisha yetu ya Unyonge tulishayazoea,sisi tubaki hivyohivyo na unyonge wetu ili mradi Amani tuwe nayo...tutafanyaje na mbu ndio wetu...wacha watung'ate.
Ebu ona kazi ya ziada inapowapata hata kina mama katika kusukuma magari ndani ya madimbwi ya maji machafu kabisaa,"Afrika bara langu siwezi kukukwepa"ila mmmh hatari sana. |
Afrika tutafika?Viongozi wetu japo mkae kwa dakika kumi kuwafikiri hawa watu wa kiwango cha chini kimaisha wanaopoteza muda wao kupanga foleni kwenye jua kali kuwachagua nyinyi halafu nyinyi haohao mnawasahau kuwa waliwachagua kwa kuwaamini mtakidhi mahitaji yao mliowaahidi."Ewe kiongozi wangu nilitumia muda wangukukaa chini na kukuchagua wewe ebu angalia ninavyoishi mimi mwananchi wako na unapoishi wewe je kweli ni haki"?
0 Comments