Shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu, Mohamed Bin Hammam(Pichani juu) na Jack Warner(Pichani chini) baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.
Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa.
Maafisa wawili wa shirikisho hilo Debbie Minguell na Jason Sylvester pia wamesimamishwa.

Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.
Petrus Damaseb,makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili, alisema haya juu ya Bin Hammam na Warner: "tumeridhika kwamba kuna majibu tunayohitaji kuhusu suala hili."
Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo.
Kama watapatikana na hatia, wanaweza kufukuzwa kutoka shirikisho hilo na kupigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu.
Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya Jumapili.