Akijibu hoja hiyo, Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi hana ubavu wa kumng’oa mwaka 2015 hata kama atavaa ‘hereni’ masikio yote mawili kwa sababu wananchi wa jimbo la Kyela wanafahamu mambo ya maendeleo aliyowaletea katika kipindi cha miaka mitano ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo.
“Sugu (Mbunge wa Mbeya Mjini) hawezi kuning’oa ubunge Kyela hata avae heleni masikio yote mawili, kwa sababu wananchi waishio Wilaya ya Kyela wanajua kupambanua, kuchana mistari na kuchochea maendeleo yao,” alisema Dk. Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alimshauri Mbunge wa Mbeya Mjini kwamba kwa kuwa bado ni mwanasiasa mchanga hivyo aelekeze nguvu zake katika kuwatumikia wananchi wa jimbo lake analoliongoza na siyo kukimbilia katika majimbo ya watu wengine kueneza propaganda ambazo haziwezi kumjenga kisiasa.
Dk. Mwakyembe alisema Mbilinyi kama mwanasiasa mchanga anayechipukia anapaswa kutambua kuwa hawezi akapata umaarufu kisiasa utakaomfanya aendelee kuaminiwa na wananchi wa Mbeya mjini kwa kwenda kwenye majimbo mengine.(source nipashe).
0 Comments