Nilikuwa nawahi kwenye msiba, foleni ikanianzia Mnazi Mmoja kwenda Airport. Tangu saa 7 nimefika Tabata saa 10.30 tena baada ya kupita vichochoroni.

Tatizo la foleni halitakaa limalizike kwa sababu serekali yetu haina vyanzo vingine vya mapato. Ukiondoa foleni kodi itokanayo na mafuta itashuka, serekali itakosa kodi. (Haya ni majibu ya kiongozi mmoja wa serekali aliyonipa wakati natoa pendekezo la kupunguza foleni Dsm)

Tukiondoa foleni, tutaongeza ufanisi makazini, tutakuwa na watu wenye afya na hata uzalishaji utaongezeka. Watu watawahi maofisini na kwenye biashara, hawatakwepa au kuondoka kazini kabla ya muda ili kuwahi foleni, nk.

Mfano; Dsm ina gari zipatazo 400,000 mbali na pikipiki. Kwa kukaa kwenye foleni saa 1 kila gari inapoteza wastani wa lita 2. Ina maana, kwa asbh na jioni tunapoteza Lts 1.6m ambazo ni wastani wa TZS 3.2 billion tunazopoteza kwa siku sababu ya foleni. Kwa mwezi ni kama TZS 96 billion na kwa mwaka ni zaidi ya Tzs 1.2 trilion.

Fedha zote hizi tunazipoteza interms of foreign currency kwa sababu lazima tutumie dola kuagiza mafuta.

Kinachonisikitisha zaidi, ninalipa mamilioni ya PAYE na kodi nyingine kwa mwaka lakini badala ya serekali kujenga miundombinu mizuri na ya kudumu, wanafikiria kuongezeana posho za safari, bunge, vikao, overtime, magari ya kifahari nk.

Kuna siku waziri mmoja alikuwa kwenye kikao na bosi wangu na wakuu wa idara kwa zaidi ya masaa matatu. Muda wote huo, gari lake aina ya V8 lilikuwa limepaki kwenye yadi yetu na lilikuwa linanguruma, dereva kalala anapulizwa na kiyoyozi. Kwa ninavyoyafahamu magari hayo unywaji wake wa mafuta, kwa masaa matatu alitumia takriban lita 7 hadi 10

Viongozi tuhurumieni basi! Tunaumia kodi zetu mnazochuma!

Serekalini zipo Land Cruisers zipatazo 800. Ningekuwa RAISI, ningeuza zote, niwape mikopo ya Rav 4 watendaji wote wanaostahili magari. Ningewapa na kadi za mafuta za BP au TOTAL zenye limit ya lita 200 kwa mwezi ambazo ni wastani wa Tzs 400,000 hadi 500,000.

Kwa kufanya hivyo, ningeondoa gharama za mafuta yanayotumiwa hovyo, ghatama za matengenezo zisingekuwepo na magari yangelindwa na kutunzwa. Kwa njia hii tungeokoa mabilioni ya hela. (800cars x 20lts per day at minimum x 2,200per liter x 30 days x 12months) = 12,672,000,000 kwenye mafuta ya gari za serekali tuu.

Bado matengenezo pale Toyota Tanzania na service ambazo gharama yake kwa mwaka inazidi hizo bn 12 za mafuta.

Turudi kwenye posho za wabunge wetu. Kila siku ya kikao cha bunge mbunge anapata posho takribani Tzs 150,000 x wabunge 320 x siku 14 = 670m kwa kikao kifupi cha wk 2. Kwenye kikao cha budget ndo usiseme. Natamani kulia machozi ya damu!!!!!

Huu ni ujinga tunaoundekeza. Ifike mahali tuone aibu kwenye hizi rasilimali za umma!

Asante japo natamani tuikodishe ikulu kwa Mjerumani na wakuu wote wa wilaya na mkoa wawe wajerumani. Tutandikwe viboko kwanza hadi tujue kujitawala. 
                       (Toka kwa mdau Semali Juda J.)