Hatua hiyo itawawezesha Wapalestina zaidi kuvuka mpaka kwa urahisi, ingawa biashara haitoruhsiwa kupita.
Israel na Misri zilifunga mpaka huo wa Gaza, tangu Hamas iliposhika madaraka katika eneo la Gaza miaka mine iliyopita.
Waandishi wa habari wanasema hiyo ni ishara ya mabadiiko makubwa ya sera ya serikali ya Misri, tangu Rais Mubarak kuondoshwa madarakani.
Mamia ya WaPalestina wamekusanyika katika ukumbi wa wasafiri katika kituo cha mpakani cha Rafah; wengine wamebeba masanduku makubwa, wakionekana kama wanaondoka kabisa.
Lakini vikwazo vimepunguzwa tu, siyo kwamba mpaka umefunguliwa kabisa.
Kwa mfano wanaume baina ya umri wa miaka 18 hadi 40 wanahitaji ruhusa ya kusafiri, na bidhaa na biashara haitoruhusiwa kuvuka mpaka.
Watu wengi, kama msafiri Mohammad, wamefurahi na hatua hiyo.
Anasema: "Tunataraji mpaka utakuwa wazi zaidi kidogo kwa watu wa Gaza, kwa sababu tuna matatatizo mengi hapa. Inshallah."
Wapalestina wakati mwengine wanaielezea Gaza kuwa "gereza kubwa kabisa duniani".
Hapo kabla Wapalestina mia tatu tu wakiruhusiwa kuvuka mpaka hapo Rafah kila siku.
Sera hii ya sasa ni ishara kuwa uongozi mpya wa Misri, unabadilisha picha ya Mashariki ya Kati.
0 Comments