Hii sehemu ni karibu na mkoa ninaokaa mimi Maganga One,kila nikipita huwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu hili daraja.kama na sisi tungetumia vyema rasilimali zetu kwanini wazungu wasije wakatufanyia haya ili kuepuka foleni na kuongeza pato la serikali kwa ufanisi wa kazi kwa muda sahihi.juu ya daraja hili kuna barabara nne zinakwenda na nne zinarudi,bado ukija chini ya daraja nako,nafikiri msomaji unajionea mwenyewe.Ni bora kuwapa wazungu TWIGA,TEMBO,DHAHABU na mengineyo wanayoondoka nayo kisirisiri ili watujengee barabara za kusaidia uchumi na maendeleo ya nchi yetu,kuliko kuwapa kidogokidogo na kwa siri kwa maslahi ya wachache. (huu ni mtazamo wangu,naomba msinihukumu).