Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiendesha Semina ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliyowashirikisha watendaji mbalimbali wa wizara na idara, iliyoanza mjini Unguja. Kushoto ni Katibu Mkuu Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu).