Kibopa nambari moja duniani Bill Gates na mai waifu wake Melinda  Gates leo wametembelea kituo cha utafiti cha Ifakara tawi la Bagamoyo kuangalia shughuli za utafiti wa chanjo ya Malaria unaofanywa na kituo hicho. Bill na Melinda Gates wametoa msaada kwa dola bilioni 10 kusaidi mapambano dhidi ya Malaria na ugonjwa wa Trachoma hivyo ni wadau muhimu hapa nchini na wanastahili heshima zote
Bill na Melinda Gates wakipata maelezo juu ya tafiti za Malaria kituoni hapo 
"Jamani sikilizeni,mpira ni akili na nguvu,hivyo ili ujue mpira lazima umsikilize sana kocha sawa"? mzee wa kuhisi nahisi kama Andy Cole mshambuliaji wa zamani wa timu tishio duniani Manchester United alikuwa akiwapa dondoo vijana wa timu ya sekondari ya Makongo leo hii.
 Andy Cole akitoa mafunzo mbalimbali juu ya kabumbu uwanjani kwa vijana wa shule ya sekondari ya Makongo.Andy Cole yupo nchini kwa kuinua kiwango cha soka letu.
Flash ni muhimu sana ili kuweka kumbukumbu,Andy Cole katikati kati ya waliosimama akipata picha ya pamoja na vijana wa Makongo sekondari leo hii baada ya mafunzo.(Picha kwa hisani ya Michuzi).