Msichana aliyekuwa ametekwa nyara Marekani Jaycee Dugard amesema kuwa alipokonywa maisha yake wakati alipotekwa nyara na Phillip na Nancy Garrido akiwa na umri wa miaka 11, na anachukia kila sekunde ya miaka yake 18 aliokuwa kwenye mazingira mabaya.
Sasa ana miaka 31, na ndio mara ya kwanza anatoa taarifa kwa uma,ambayo ilisomwa mahakamani na mama yake, wakati mume na mke waliokuwa wamemteka wakihukumiwa kwa kupatikana na hatia ya utekaji nyara na ubakaji.
Nancy Garrido, 55, alihukumiwa kifungo cha miaka 36 hadi maisha,na mumewe kifungo cha miaka 431.
Phillip Garrido, sasa ana miaka 60, alipata watoto wawili na msichana huyo.
Dugard aliwekwa na watoto wake wawili wa kike,sasa wana umri wa miaka 13 na 16,nyuma ya nyumba ya Garrido huko Antioch, California, akiwa kwenye hema.
Mwezi Aprili watu hao walikiri kufanya makosa, hii inamaanisha kuwa Dugard hakuhitajika kufika mahakamani.
Kama sehemu ya makubaliano waliokubaliana na mwendesha mashtaka,wote walikubali kutokuwa na haki yao ya kukata rufaa.
Jaji alielezea namna walivyomfanya Dugard kama ukatili na jambo lililokubalika.
Wakili wa Nancy Garrido, Stephen Tapson, aliomba kwamba aruhusiwe kumuona mumewe kwa mara ya mwisho na aruhusiwe kuwa mahakamani wakati wa hukumu yake kusomwa, lakini jaji alikataa,shirika la habari la AFP lilisema.