Kutokana na uwezo wa mboni zetu za macho kuwa hafifu huwa hatuoni vitu gani vinarushwa hewani na mpiga chafya.
 Ndio maana unaambiwa mafua yanaambukiza,jitahidi sana unapomuona mtu anapiga chafya ujisogeze mbali kidogo kwani usipofanya hivyo kwa kuona haya ujue unaambukizwa virusi vya mafua.
Inashauriwa sana kujitahidi kuiziba chafya yako kwa kitambaa,na kama huna kitambaa kwa wakati ule au chafya imekujia kwa haraka sana basi jitahidi kuinamisha kichwa chako chini ili kuepusha maambikizi ya virusi vyako kwa wenzako.Huu ni ushauri wangu,Maganga One.