Makundi mengi ya kimataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu yaliwekewa marufuku katika maeneo yote ya Somalia chini ya uthibiti wa kundi la Al Shabaab linaloaminika kuwa na uhusiano na mtandao wa al Qaeda.
Lakini mashirika wanachama wa kamati ya kimataifa inayoshughulika na majanga DEC yanajiandaa kuimarisha shughuli za misaada kusini mwa Somalia huku maelfu ya raia wakiendelea kukimbia nchi za Kenya na Ethiopia pamoja na mji wa Mogadishu kutokana na ukame.
Ni wiki jana ambapo kundi la Al Shabaab lilitangaza kuoandoa marufu yake kwa mashirika ya kigeni yanayotoa misaada kufuatia hali mbaya ya ukame. Ni kutokana na mwaliko huu ambapo mashirika ya misaada yananuia kuchukua nafasi kuwasaidia raia wa Somalia japo mpango mpya wa Al Shabaab ungali kupata imani ya wengi.
Kundi hili tayari limeorodheshwa kama la kigaidi na mataifa ya Marekani na Uingereza. Aidha baadhi ya nchi wafadhili zimeelezea hofu kwamba huenda chakula cha misaada kikaelekezwa kuwafaidi wapiganaji wa kiisilamu wa Al Shabaab.
0 Comments