Huyu ndiye mama Sharon au mama Roshan,mke wa Maganga One,Jana amesheherekea siku ya kuzaliwa kwake.Pichani akiwa ameshika keki ili kuileta watu Tuifaidi,Keki ilikuwa tamu jamani haielezeki.
 Jamani keki tamu kweli......yani tumeila mpaka basi..
Kata keki mke wangu,kata keki mama Sharon,kata keki mama Roshan kata keki tulee..
 Wacha weeeee,kula bwana kulaaaaaa,kula mume wangu kulaa, kula baba watoto, hapo mke wangu ananilisha kipande cha keki,Hongera mke wangu kwa siku ya kuzaliwa kwako.
Mke wangu na mdogo wake,hapo mdogo mtu akilisha keki bidada.
Kula mwanangu kulaaa,Mama mtu akimlisha mtoto wake Sharon keki.....
Haya kula mdogo wangu kulaaaa,mabidada wakipata flash huku full tabasamu,ilikuwa burrrdan sana..
Kula bidadaa kulaaa,yani mama sharon leo kajua kudeka,wadogo zake walikuwa wakimlisha tu...
Waaawww!!!!,toka kushoto ni Sharon bint yetu wa Kwanza,mimi(Maganga One),mke wangu mama  Sharon na last born wetu binti yetu Roshan.
 Hapo ni full salad,ilikuwa ni kujichana kwa kwenda mbele.
 Mamma miaa hii kitu inaitwa Samoosa ila waswahili wanaita SAMBUSA....
 Ebwanaa eeeh hii kitu naipendaaa ila jina lake ndio sijui tunaitaje,BADIA,BAJIA au BAGIA...
 Hawa ni kwioooooo ni vunja mifupa tu.
Ndizi mzuzu za kukaanga hapoooooo..............
Waswahili bwanaa,hatuachi asili yetu...meza zipo ila chini kama kawaida tu....Kila mmoja full smile hadi raha.
Hapo kila mmoja ni bize kivyake,yani full purukushani.....

 Wacha weeee,mama Sharon na mama Fahad hapooooo

 MASH`ALLAH  MKE WANGU,MWENYEZI MUNGU AKUJAALIE KILA LA HERI KATIKA UHAI WAKO WOTE ULIOBAKI,AKUSAMEHE MAKOSA YAKO UNAYOYAJUA NA USIYOYAJUA,TUPENDANE MILELE.
 Hapo napo,mama Sharon na Aunt Sharon wakipata flash kuweka kumbukumbu ..
 Mdogo wangu Pasua kichwa(baba fahad)nae hakubaki nyuma kwenye kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa shemeji yake mama Sharon.
 WAPENDANAO HAOOO  ,HAPA NI KUZAMA KUZUKA..MAGANGA ONE NA MKE WANGU KIPENZI MAMA SHARON.MWENYEZI MUNGU ATULINDIE NDOA YETU INSH'ALLAH.
Leo ni siku ya kuzaliwa kwako mke wangu,nakutakia kila la heri katika maisha yako,Mungu akulinde na shari zote,Mungu akuzidishie wema na mapenzi yako ya ukweli kwangu,lea watoto wetu vyema...Tupendane zaidi na zaidi.Hongera sana na nakupenda mke wangu.....Maganga One.