Nelson mandela ambaye kwa sasa ni myonge kiafya amekuwa chini ya uanagilizi wa karibu kutoka kwa madakatari kwa muda wa saa 24 tangu atoke hospitali mwezi januari pale alipolazwa baada ya kuugua.

Lakini hali hii haijawazuia raia wa Afrika Kusini na watu wengi duniani kumtakia kheri njema anavyo sheherekea miaka 93 tangu azaliwe.

Watoto wakila keki ya birthday ya kuzaliwa kwa mzee Nelson Mandela.

Kuadhimisha siku hii, nyimbo maalum imetungwa kwa heshima yake.

Raia wa Afrika kusini wanatarajia kuweka historia ambapo yamkini watu milioni 12 wataimba wimbo huo kwa wakati mmoja.


Shirika la utangazaji nchini humo (SABC) pamoja na idara ya elimu wamefanya mapango kuwa ifikiapo saa mbili na dakika tangu asubuhi hii, wanafaunzi katika shule zote nchini watauimba wimbo huo maalum uliotungwa kwa heshima ya Madiba.

Siku hii ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela, rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini ni siku ya kimataifa iliorodheshwa na Umoja wa Mataifa.

Nchini Afrika Kusini kila mtu atajitolea dakika 67 za muda wake leo kufanya huduma za kijamii.

Viongozi mbali mbali duniani wamemtumia salamu za kheri njema mzee Mandela wakiongozwa na Rais Barack Obama wa Marekani.

Rais Obama amesema Mandela ni nembo ya demokrasia na haki duniani na amemshukuru kwa kujitolea maisha yake kwa huduma ya jamii.

Kiongozi huyo wa marekani amesema Mandela ataacha urithi wa busara, nguvu na fadhila nyingi.