Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen amelihutubia taifa lake kwa njia ya televisheni kwa mara ya kwanza tangu kuungua katika shambulio liliofanywa katika kasri yake mwezi uliopita.
Bw Saleh amekuwa akifanyiwa matibabu nchini Saudi Arabia tangu tarehe 6 Juni baada ya shambulio ambalo wakuu wa serikali ya nchi hiyo walisema yalisababishwa na bomu.
Akiongea kutoka Saudi Arabia Rais Saleh amesema amefanyiwa operesheni nane kutibu majeraha ya kuungua na kwamba zote zimefanikiwa.
Mikono yake ilikuwa imefungwa bandeji na alisisitiza haja ya mazungumzo ili kuyatanzua matatizo ya Yemen.
Kwa muda wa miezi kadhaa sasa Yemen imekumbwa na machafuko, huku waandamanaji wakidai Bw Saleh ajiuzulu.
Lakini amekataa kujiuzulu na amezipuuza juhudi zote za kuleta upatanishi kati yake na waandamanaji.

0 Comments