Mhariri Mkuu wa gazeti la HABARILEO, Joseph Kulangwa akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari Gerezani, Dar es Salaam namna habari zinavyokusanywa kutoka sehemu mbalimbali nchini na duniani kote na kuzichapisha kwenye gazeti. Kutoka kushoto ni Abdulhamid Masoud, Shabani Said, Michael Msingi na Omary Seif. Wanafunzi hao walitembelea Ofisi za Magazeti ya Serikali ya Daily News, Sunday News, HABARILEO na HABARILEO JUMAPILI (TSN) ili kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu magazeti hayo. (Picha na Yusuf Badi).