BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro, linatarajia kutoa tamko lake juu ya kondoo aliyezaliwa akiwa na maandishi ya Koran.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Shehe Rashid Malya, alipozungumza na gazeti hili baada ya kikao kilichokuwa kitoe tamko hilo jana kuahirishwa.
Kuahirishwa huko kulitokana na Shehe wa Mkoa ambaye alikuwa asimamie kikao hicho kushindwa kufanya hivyo, kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.
Awali ilibainishwa kuwa mashehe wa mkoa huo walikuwa wakutane wajadili kuhusu kondoo huyo na kisha kumpa tamko Shehe wa Mkoa na kuliwasilisha kwa jopo la wasomi ambao ndio wangetoa tamko rasmi kuhusu majaaliwa hayo.
Kondoo huyo aliyezaliwa Julai 6 amekuwa kivutio kikubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, ambapo hadi sasa watu kutoka mikoa ya Dar es Saalam, Tanga na Arusha wamefika kushuhudia maajabu hayo.
Hadi sasa pamoja na watu kumiminika katika kijiji cha Uduru wilayani Hai kumshuhudia, kuna watu wamejitokeza kutaka kumnunua kwa hata Sh milioni 10 lakini mmiliki wake, Grace Masawe, anasema hayuko tayari kumwuza.
Alieleza sababu za kukataa kumwuza kondoo huyo, kuwa ni kutokana na familia yake kutojua nini maana ya tukio hilo na kwamba inachukulia kitendo hicho kama baraka kwa familia.

Maandishi aliyonayo kondoo huyo yana maana ya Yasini ambayo ni moja ya aya muhimu katika Koran pia ni moyo wa Kitabu hicho.
“Aya hii ni moyo wa Kitabu Kitakatifu cha Koran, kinachoelezea mambo mengi makubwa hususani nyakati za mwisho … inaonesha ishara kuwa hizi ni siku za mwisho za kiyama,” alisema Shehe Malya.
Alisema aya ya maandishi hayo katika Koran ni moja ya sura zinazoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa Kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiyama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake.
Aliongeza kuwa hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, kwa sababu Kitabu Kitakatifu cha Koran kilishushwa Mwezi wa Ramadhan, hivyo ishara hii katika kipindi cha Mfungo Mtukufu wa Ramadhani ni kubwa.
Pia Shehe Malya aliongeza kuwa neno Yasini ni jina lingine la Mtume Muhammad (SAW) alilopewa na Mwenyezi Mungu, na kueleza kuwa hiyo ni miujiza na bahati kwa dini hiyo.
“Haya maandishi katika aya ya Kitabu cha Koran yamejikita zaidi kuonesha hizi ni siku za mwisho za kiyama, hivyo wakati huo midomo haitaongea tena ila mikono itasema na miguu itashuhudia, hivyo Mungu akipenda jambo lake liwe linakuwa,” alisema Shehe Malya.
Grace alisema familia inayomiliki kondoo huyo ni ya Kikristo, ingawa ameibuka mmoja wa wanafamilia, Said Masawe na kusema si kweli kwamba familia hiyo ni ya Kikristo bali ni mchanganyiko wa Wakristo na Waislamu.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi, Masawe alisema hatua ya kusema kuwa familia hiyo ni ya Kikristo pekee, imesababisha manung’uniko ndani ya familia kwa vile haijawatendea haki wanafamilia Waislamu.
“Familia yetu ni ya mchanganyiko wa dini mbili za Uislamu na Ukristo. Pale nyumbani alipo yule kondoo, mwenye mji ni marehemu babu yetu Mzee Said Masawe, ambaye mimi ndiye nilirithi jina lake. Babu alikuwa Mwislamu na hata marehemu mkewe, yaani bibi pia alikuwa Mwislamu jina lake ni Mwanaidi Masawe.
“Si hao tu, hata baba mkubwa Khalifa Masawe anayeishi Monduli ambaye alikuwa pale nyumbani, baada ya kuzaliwa kwa kondoo yule, ni Mwislamu. Alikuwapo pia marehemu baba yetu mkubwa marehemu Suleiman Masawe, ambaye ni Mwislamu. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Waislamu ndani ya familia tupo wengi tu ingawa na Wakristo pia wapo,” alisema Masawe.
Alisema mama yake anayeishi katika makazi hayo kwa hivi sasa ambaye ndiye aliyelieleza gazeti hili, kuwa familia yao ni ya Kikristo, Grace (55), alizungumzia imani yake yeye binafsi, kwani ni Mkristo, lakini hiyo haina maana kuwa wanafamilia wote ni Wakristo.
“Hivi sasa baada ya tukio, baba mkubwa (Khalifa), ametutaarifu wanafamilia wote lakini kwa vile tukio limetokea wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tumekubaliana kwamba baada ya funga, wakati wa Sikukuu ya Idd wote tuwe Moshi ili tusome dua na kumaliza kila kitu kwa jambo hili la ajabu lililotokea,” alisema Masawe.
0 Comments