Vijana wengi hivi sasa kisiwani Zanzibar wamekuwa na mambo ya kuiga utumiaji wa madawa ya kulevya kama unavyojionea pichani,baada ya kuona raha haitoshi kujitoboa na sindano mkononi anaamua kupata raha ya chapchap shingoni.
 Mtu mzima wa makamo ambaye hajali wala kuthamini familia yake nyumbani,matokeo yake anajimaliza mwenyewe na madawa ya kulevya.
Ebu ona jinsi hawa watu walivyo na hatari,sijui wamesomea wapi jinsi ya kuitafuta mishipa ambayo kwao ni rahisi kwa kupenyeza sindano yenye sumu ya madawa hayo.
 Kijana mdogo kabisaa,badala ya kuchakarika kutafuta kazi na kulijenga taifa lao matokeo yake ni kama unavyojionea hapo pichani,yeye na madawa na madawa na yeye.
 Ebu ona jinsi walivyowataalamu wa matumizi ya madawa hayo,kila aina ya mishipa wanaijua wao.
Kwa jinsi Zanzibar ilivyochafuka si wasichana au wavulana wenye kujitapa kwamba wao ni zaidi,siku hizi wote ni ngoma droo kwa matumizi ya cocaine.
Mwingine akiona anacheleweshwa kudungwa sindano basi ujidunga mwenyeweee.Kiukweli Baadhi ya wananchi wanalalamika sana juu ya Jeshi zima kuhusiana na kutokuwa na umakini kwa wanaoingiza madawa hayo kisiwani huko.