Rais wa Fifa Sepp Blatter kushoto,Pele mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Rais wa Brazil Dilma Rousseff.

Rais wa Fifa Sepp Blatter siku ya Jumamosi ya tarehe 30 Julai, alihudhuria sherehe ya kifahari za kupanga nchi katika makundi ambazo zitakazoshiriki kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika katika ufukwe wa pwani ya Copacabana mjini Rio nchini Brazil. Uchumi wa Brazil unakuwa kwa haraka, lakini patashika za kuelekea Kombe la Dunia hata hivyo zinaonekana kuchochea zaidi maendeleo ya uchumi.
Hivi sasa barabara mpya zinajengwa, viwanja vya ndege navyo vinaanza kupata sura mpya inayohitajika. Kumekuwa na kuchelewa kwa hapa na pale, lakini waandalizi hivi sasa wameonesha matumaini katika kazi za maandalizi. Na tofauti na uamuzi wa kuizawadia Qatar nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2022, kwa Brazil kupata nafasi hiyo ya kuandaa, hakuna cha kutiliwa mashaka kwani kandanda ndio nyumbani kwake Brazil.

Tuangalie nchi za Afrika zilivyopangwa.
Mzunguko wa kwanza utakayo kuwa na mechi 12 za nyumbani na ugenini kati ya tarehe 11 hadi 15 mwezi wa Novemba, ambapo washindi watasonga mbele katika patashika za mzunguko wa pili.
Seychelles na Kenya
Guinea Bissau na Togo
Djibouti na Namibia
Mauritius na Liberia
Visiwa vya Comoro na Msumbiji
Equatorial Guinea na Madagascar
Somalia na Ethiopia
Lesotho na Burundi
Eritrea na Rwanda
Swaziland na jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Visiwa vya Sao Tome na Principe na Congo
Chad na Tanzania
- - -

Kwa makundi nchi hizo zimepangwa hivi:
Kundi A
Afrika Kusini
Botswana
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Somalia na Ethiopia
- - -
Kundi B
Tunisia, Visiwa vya Cape Verde, Sierra Leone, Equatorila Guinea na Madagascar

- - -
Kundi C
Ivory Coast
Morocco
Gambia
Chad/Tanzania
- - -
Kundi D
Ghana
Zambia
Sudan
Lesotho/Burundi
- - -
Kundi E
Burkina Faso
Gabon
Niger
Sao Tome and Principe/Congo
- - -
Kundi F
Nigeria
Malawi
Seychelles/ Kenya
Djibouti/Namibia
- - -
Kundi G
Egypt
Guinea
Zimbabwe
Comoros Islands/Msumbiji
- - -
Kundi H
Algeria
Mali
Benin
Eritrea/ Rwanda
- - -
Kundi I
Cameroon
Libya
Guinea Bissau/Togo
Swaziland/Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
- - -
Kundi J
Senegal
Uganda
Angola
Mauritius/Liberia
Mechi zitachezwa kati ya tarehe 1 mwezi wa Juni, 2012 na tarehe 10 mwezi wa Septemba 10, 2013.

Washindi wa kila kundi watasonga mbele hadi raundi ya tatu, wakicheza mechi za nyumbani na ugenini kati ya tareh 11 hadi 15 mwezi wa Oktoba, 2013 na washindi ndio watafuzu kucheza katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.