Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton amezitaka serikali nyingine za magharibi kuiwekea vikwazo nchi ya Syria kufuatia harakati za kijeshi dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali.
Amesema hatua kutoka Ulaya, China na India zinaweza kuathiri sekta ya nishati nchini Syria na kumshinikiza rais Bashar Al Asaad.
Jumatano wiki hii Marekani ilitangaza kuiwekea vikwazo nchi ya Syria. Hata hivyo utawala wa Rais Obama anafahamu kwamba baadhi ya serikali za magharibi zina uhusiano wa ndani na Damascus na inataka zichangie kuhusu mzozo wa Syria.
Kwenye mahojiano na shirika la habari la CBS NEWS, Hillary Clinton alitangaza wazi kuitaka Urusi iwache kumuuzia rais Bashar Al Asaad silaha. Aidha ametaka vikwazo vipya kulenga sekta ya nishati moja wapo ya tegemeo kubwa la mapato kwa serikali ya Syria.
Hapo Alhamisi Rais Barack Obama alifanya mazungumo kwa njiya ya simu na Waziri Mkuu wa Uturiki Recep Tayyip Erdogan. Msemaji wa ikulu ya White house amesema viongozi hao waliafikiana kwamba sharti umwagikaji wa damu kusitishwa mara moja na Syria kuanza mchakato wa mageuzi ya kidemokrasia.
Vyombo vya habari Marekani vimesema rais Barack Obama anajitayarisha kutoa tangazo la kumtaka Bashar Al Asaad kuondoka madarakani. Msemaji wa rais amewaambia waandishi habari kwamba muda wa utawala wa bw. Asaad umefika kikomo na kwamba dunia itakuwa salama bila kuwa na viongozi kama yeye.
0 Comments