Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, kuhudhulia Fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur-an tukufu iliyofanyika kwenye ukumbi huo na kuwashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Diamondi Jubilee jijini Dar es Salaam leo wakifuatilia kwa makini fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma Hotuba yake wakati wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo na kushirikisha jumla ya wshiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo,Jahuddin Adam, kutoka Sudan akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi wa fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo, Kombo Bahi Makame kutoka Unguja-Tanzania, akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi katika fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano hayo,Mohammad Sad Tawfiq, kutoka Egypt akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo, ambapo mgeni rasmi wa fainali hizo zilizowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mshiriki kutoka Tanzania, Ibrahim Ramadhan, akishiriki fainali za mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Jahuddin Adam, kutoka Sudan,baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kutangazwa washindi katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo.
0 Comments