Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametangaza baraza lake la mawaziri
Hilo ni baraza la kwanza la mawaziri tangu Sudan Kusini kupata uhuru mwezi uliopita.

Wizara 29 zimegawiwa karibu sawasawa baina ya maeneo matatu makubwa ya nchi.

Mwandishi wa BBC mjini Juba, anasema ilikuwa shida kuteua mawaziri, kwa sababu ya mvutano baina ya makabila ya nchi hiyo.

Rais Salva Kiir angeweza kulaumiwa kuwa anapendelea kabila lake la Dinka, lakini inaonesha amewaridhisha wale wanaomlaumu.

Kwa sababu ya kuweka mezani ya makabila inamaanisha kuwa maafisa wa daraja za juu wa vita vya ukombozi, hawakupata nyadhifa, akiwemo katibu mkuu wa chama tawala, Pagan Amum, na naibu wake, Anne Itto.