Rais Barack Obama ametangaza kuwa viongozi wa chama cha Republican na chake cha Democratic wameafikiana kuhusu mpango wa kulipia deni la serikali.
Bw Obama amesema chini ya makubaliano hayo nchi hiyo itapunguza matumizi yake kwa dollar trilioni moja katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Hata hivyo mpango huo utapigiwa kura kwenye baraza za senate hii leo.
Muafaka huo umefikiwa ikiwa imebakia siku moja tuu kabla ya makataa ya kuongeza kiwango cha kukopa fedha za kulipia madeni yake.
Kwa wiki kadhaa, viongozi wa vyama hivyo wamekuwa wakivutana kuhusu njia bora ya kufuata kukabili madeni ya marekani.
Hali ambayo ilitishia kukwamihsa shughuli za serikali.
Baraza la senate lina hadi kesho kupiga kura kuongeza kiwango hicho cha kukopa hadi dola trilioni 14 lau sivyo shughuli za serikali zitakwama.
Rais Obama amesema kuwa mpango ulioafikiwa sio ule aliotarajia lakini amelazimika kuukubali ilikuwezesha huduma za serikali kuendelea na madeni yake yalipwe.
Utawala wa Rais Obama ulikuwa unakabiliwa na shinikizo kali kutoka kwa wapinzani kutoka chama cha Republican ambao walikuwa wanapinga pendekezo lake la kuwepo na mpango ambao utasitiri hali hadi mwisho wa mwaka ujao.
Chama cha Republicans kilitaka mpango huo uwepo hadi katikati ya mwaka ujao. Lakini sasa vyama hivyo vimekubaliana kuunda kamati maalum itakayotoa mapendekezo mapya mwezi Novemba.
0 Comments