WAKATI wafanyabiashara wa mafuta nchini wamesisitiza kwamba wataendelea na mgomo wao hadi bei itakapoongezwa, Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta na Maji (EWURA) imesema itafuta leseni kwa kampuni zitakazoendelea kugoma.
Kwa nyakati tofauti jana, Ewura na wamiliki hao kupitia Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta ya Petroli nchini (TAOMAC), walifanya mikutano na waandishi wa habari Dar es Salaam na kusisitiza misimamo yao huku kila upande ukisema kamwe hautatii agizo la upande mwingine.
Mkurugenzi Mtendaji wa TAOMAC, Salum Bisarara, alisema kampuni zote za mafuta hazitaendelea kuuza mafuta kwa bei kikomo ya Sh 2004 kama ilivyoagizwa na Ewura, kwa vile bei hiyo inasababisha hasara ya kati ya Sh 150 na Sh 250 kwa lita jambo ambalo alisema haliwezi kuvumilikaAlisema ingawa wamiliki wa kampuni za mafuta wamekuwa wakitoa nafasi kwa Ewura ili kurekebisha kasoro zilizopo katika okokotoaji wa upangaji wa tozo za mafuta ili kuepusha hasara kwa kampuni hizo, Ewura wameshindwa kufanya hivyo hatua iliyowafanya wagome.
Alitaja maeneo yenye matatizo kuwa ni Ewura kukataa kukubaliana na bei ya ununuzi wa mafuta kwenye Soko la Dunia (FOB) kama inavyotajwa na waagizaji hao, kuondoa asilimia 7.5 iliyokuwa inatolewa kwa kampuni hizo, ili kufidia hasara wanazopata katika mlolongo wa uagizaji wa mafuta, usafirishaji na upakuaji, gharama za ubadilishaji wa fedha za ndani ili kupata fedha za kigeni za kuagizia mafuta na muda mrefu unaotumika kuruhusu meli kushusha mzigo bandarini.

Alisema vipengele vyote hivyo kwa pamoja, ndivyo vinavyofanya kampuni hizo kugoma kuuza mafuta kwa bei kikomo iliyowekwa na Serikali, kwa vile ukokotoaji wa gharama zote zinazotumika katika vipengele hivyo, pamoja na riba zinazotozwa na benki kwa kampuni hizo zinapokopa fedha za kuagiza mafuta, unaonesha wazi hasara inayopatikana.
“Watu wanaangalia hili suala kwa juujuu. Hebu chukua hasara ya Sh 150 au Sh 250 kwa kila lita, halafu zidisha mara lita milioni moja au milioni tano zinazouzwa kwa siku, utaona namna kampuni hizi zinavyopata hasara kubwa.
“Wanaweza kusema tuuze mafuta kwa lazima na hata kwa mtutu wa bunduki, lakini yatakapokwisha kwenye visima nini kitafuata, maana kampuni zitakuwa zimepata hasara na kushindwa kuagiza mafuta mengine na nchi itafika mahala pabaya.
Kwa bei hii waliyoweka mwezi mmoja ni mkubwa sana, kampuni zote za mafuta zitakuwa zimefilisika,” alisema Bisarara.
Alisema ili kununua lita 35,000 za mafuta za kutosha meli moja, kampuni hizo hutumia Sh bilioni 50 ambazo hukopwa benki na kutakiwa kulipwa pamoja na riba, lakini pia mafuta mengi hasa petroli, huyeyuka wakati wa usafirishaji, mengine hupotea wakati wa kushusha na pia kampuni hizo hupata hasara kubwa wakati wa meli kusubiri kushusha mafuta ambapo hutumia kati ya siku 45 na 60, jambo ambalo Ewura wanapaswa kulifanyia kazi katika ukokotoaji wa tozo ili kupanga bei mpya.
“Si hilo tu, lakini pia kuna tatizo la ukubwa wa bei ya dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania, hatua inayotupa hasara kubwa wakati wa kununua dola, maana mafuta tunauza kwa bei ya Tanzania, lakini tunapoagiza ni lazima tutumie dola.
“Kuna tatizo pia la gharama za uendeshaji na kodi ambazo ziko juu sana na pia lipo tatizo la mita ya kusoma kiwango cha mafuta, ambalo kesi yake ipo mahakamani sasa. “Ni vizuri kama suala hili litaangaliwa kwa kina na si kutuona kama sisi ni wabinafsi, si wazalendo na tusiowatakia mema Watanzania,” alisema Bisarara.
Hata hivyo, Ewura walijibu mapigo hayo, kwa kuzitaka kampuni hizo kuendelea kuuza mafuta kwa bei hiyo mpya, huku Mkurugenzi Mkuu, Haruna Masebu, akionya kuwa kampuni zitakazokaidi kufanya hivyo kuanzia jana, zitapokonywa leseni za biashara mara moja.
Masebu aliwaambia waandishi wa habari, kwamba si kweli kwamba kampuni hizo zinapata hasara kama zinavyodai na kwamba mlolongo mzima wa ununuzi, usafirishaji, ushushaji na utozaji wa tozo, viko wazi na vinaweka bayana gharama zote zinazotumika katika biashara ya mafuta.
“Si kweli kwamba wanapata hasara. Hebu angalia kama jana na leo (juzi na jana) wakati kampuni hizi kubwa zilipogoma, zipo kampuni ndogo za mafuta ziliendelea kuuza mafuta kwa bei hii mpya. Hii inaonesha kwamba si kweli kwamba hakuna faida, kwani hawa wengine wangegoma pia,” alisema Masebu.
Alisema hata hivyo katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura kilichofanyika jana, kiliazimia kurekebisha maeneo mawili katika fomula ya utozaji tozo, kwa kukubali kuziongeza kampuni za mafuta kiwango cha gawio la faida kutoka Sh 108 hadi Sh 110 na pia kuwaongeza siku za meli kutotozwa kodi zinaposubiri zamu ya kushusha mafuta bandarini kutoka siku tatu hadi siku 15.
“Si kweli kwamba mfumo huu mpya wa upangaji wa bei ya petroli tumeufanya kwa kukurupuka. Ni suala lililofanywa kitaalamu na tulizishirikisha kampuni hizi kwa kiwango kikubwa sana.
“Ukiangalia nafuu tuliyoiweka katika maeneo yote, utaona ni ile inayozihusu mamlaka za Serikali zinazohusiana na usimamizi wa uingizaji wa mafuta. Tulipokuwa tunagusa ili kupunguza kitu chochote kutoka katika vipengele vinavyozihusu kampuni, walikuwa wanakataa. Punguzo kubwa limetoka kwenye ile asilimia 2.6 ambayo inakwenda kwenye Mamlaka,” alisema Masebu.
Pamoja na kusisitiza kutoongezwa kwa bei, Masebu alisema Ewura itawachukulia hatua kali wamiliki wa kampuni za mafuta wanaoonekana kushinikiza wenzao kukaidi amri za Serikali kwa vile ni kosa kisheria, wamiliki hao kukutana na kujadiliana juu ya uendeshaji wa biashara hiyo.
Alisema Ewura kwa kuanzia itamchunguza kisheria Mkurugenzi wa Kampuni ya Engen, Seelan Naidoo, kwa kutoa matamshi yanayoashiria kupinga uamuzi wa Serikali katika kukabiliana na suala la kupanda kwa gharama za mafuta.
“Yaliyopita tutaachana nayo, lakini kuanzia leo (jana) tutapita kila mahali kuangalia, kwa wale watakaogoma kuuza mafuta tutawafutia leseni mara moja na kwa watakaokutwa wakiuza kwa bei tofauti na hii yetu, tutawatoza faini ya Sh milioni tatu kila siku,” alisema Masebu.
.
0 Comments