Tuna Mlima mzuri na mrefu ambao nchi nyingi za Ulaya hawana,tuna wanyama kama Twiga ambao wenzetu hawana wanafanya kuja kushangaa nchi kwetu.
Wenzetu wana mabasi kama haya ambayo sisi kwa nchini kwetu kuyaona ni nadra na si wote ambao mnaweza kubahatika kuja kufanya utalii wa kuyaona haya mabasi,kwa kawaida neno Utalii kwa wengi wetu hatulitumii hipasavyo.
Mambo kama haya ambayo kwa mtu kama mimi hutumia muda wangu kushangaa nikiona njiani,kwani kwetu kuona vitu kama hivi ni Nadra.
Hata hapa napo naweza kusimama na kujiuliza mara mbilimbili ni akili ipi mtu ameitumia kubuni kitu kama hiki,kuna vitu vingi sana wazungu wanapokuja Afrika nao hushangazwa navyo,kwa mfano kukatika kwa umeme siku nzima,achilia mbali mgao wa kila siku kwani kitu kukatika umeme kwa nchi za wenzetu ni naweza kusema hakuna,labda, labda kama kuna matengenezo muhimu sehemu fulani na tena mmeshapewa taarifa kwa maandishi miezi mitatu kabla, hivyo mnajiandaa kwa taarifa hiyo,na tena umeme ukatwa kwa muda mfupi tu haiwezi kufika hata masaa 6.
Kwa kuwa wanyama kama hawa wenzetu hawana nao huchukua likizo toka nchi zao na kuja kushangaa kwa macho yao.Wenzetu hujifunza mengi sana kutokana na utalii wao,tofauti kubwa sana kati yao na sisi ni katika uulizaji wa maswali kwa kila wanachokiona,sisi hubaki kushangaa bila kuuliza maswali kwa kuhofia tutaonekana washamba na tunabaki na ushamba wetu.
Ardhi ya Asili yenye wanyama tofauti wa kupendeza,cha kushangaza ukijaribu kupitia Zoo zao(Mabanda yao ya maonyesho utasita ajabu kuwaona wanyama kama hawa nao wapo)Huwezi kuuliza swali kama wamewapata wapi ikiwa unajua ukweli na jibu la swali lako unakuwa nalo moyoni.
Wenzetu wana mabustani mazuri ya kupendeza ila sisi tuna vitu kama hivi vya kuvutia ambavyo kwao ni agharabu kuviona.
Cha ajabu wamejaaliwa BARIDI ya ajabu mpaka mabarafu utasema wamezaliwa na mafriza,kwa upande wetu ni tofauti kuna JOTO la ajabu utasema tumezaliwa na makaa ya moto,kingine cha kushangaza Mzungu anapenda JOTO ila sisi hatupendi BARIDI.
Yani hapa huwa sichoki kushangaa,hivi utanilaumu au kuniona mshamba nikipiga picha sehemu kama hizi? huwa najiona mshamba pale nikisimama na kuangalia tukiwa na uzinduzi wa vijidaraja vyetu uchwara,ebu ona wenzetu wanavyojua nini maana ya neno usafirishaji....!!!
Hili sio barafu jamani ni jumba analoishi mwanadamu mwenzetu kama wewe na wala sio FISADI wala nini.Ukishangaa kitu kama hiki kuna tatizo?
Wanaposema tembea ujionee nami nakubali,hapa sina cha kuongea sana just angalia kwa macho tu na kutikisa kichwa chako.
Kila siku najiuliza maswali ambayo sipati jibu,mimi kama mimi nikijisifia nchini kwangu kuna Twiga,Tembo,Swala,Viboko,Vifaru,Simba na kuna Mlima Mrefu kuliko yote barani Afrika inanisaidia nini au napata faida gani?kama kawaida yangu NAZIKAANGA MBUYU HAYA WENYE MENO.............
0 Comments