Wakuu wa Afghanistan wanasema wanajeshi 31 wa Marekani na wanajeshi kadha wa Afghanistan walikufa, wakati helikopta yao ilipoanguka mashariki mwa nchi hiyo.
Hiyo ni hasara kubwa kabisa kuifika Marekani katika tukio moja nchini Afghanistan.
Helikopta hiyo iliyobeba wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani, ilikuwa katika shughuli za kupambana na ugaidi katika jimbo la Wardak.
Rais Obama alisema vifo hivo vinakumbusha Wamarekani kuwa jeshi linajitolea kwa kiwango kikubwa.
Katibu Mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, alisema, amesikitishwa sana.
Msemaji wa Taliban alieleza kuwa wao wameidungua helikopta hiyo.
Msemaji wa Taliban alieleza kuwa wao waliidungua helikopta hiyo, baada ya jeshi la NATO kushambulia nyumba ambamo wapiganaji walikuwa wanakusanyika.
NATO inasema inachunguza sababu za ndege hiyo kuanguka.
.