Picha haihusiani na maelezo.

POLISI inafanya uchunguzi kubaini sababu za mkazi wa Buguruni, Dk. Kelvin Ndimbo (51) kujinyonga huku akiwa ameacha ujumbe wa maandishi akitaka mtu yeyote asihusishwe na kifo chake.

Ndimbo ambaye polisi imesema alikuwa ni daktari aliyekuwa akimiliki duka la dawa jijini ambalo halikutajwa jina, alikutwa amekufa chumbani kwake Septemba 7 saa 11 jioni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba kwa mujibu wa ndugu zake, alikuwa akiishi bila ya mke wala mtoto.

Alikutwa amejinyonga kwa kamba ya manila.

Alisema kwamba dada wa marehemu, Felicia Ndimbo, aliacha ujumbe wa maandishi usemao ‘ndugu, jamaa, mtu yeyote asihusishwe na kifo changu, nimeamua mimi mwenyewe’.

Shilogile alisema kulingana na maelezo ya dada huyo, ndugu yao alikuwa hana mawasiliano mazuri na ndugu zake.

Mwili wake ulikuwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi unaendelea.