Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umeandaa kongamano kuangazia mustakabhali wa Somalia ndani ya nchi hiyo.
Kongamano hilo ambalo lilianza jana mjini Mogadishu, linajumuisha makundi tofauti kando na lile la Alshabaab kuangazia jinsi ya mchakato wa amani.
Mkutano huo wa kimataifa ambao unajumuisha wawakilishi wa serikali kadhaa na pia mashirika ya Umoja wa Mataifa na viongozi wa makundi mbali mbali nchini Somalia unatarajiwa kumalizika hapo kesho.