Watawala wa mpito wa Libya, baraza la mipto la taifa, wamesema majeshi yao kwa sasa yanadhibiti eneo kubwa la mji wa Sabha, kilomita 750 kusini mwa Tripoli.
Walisema wamefika katikati ya mji lakini bado kulikuwa na mapambano katika baadhi ya maeneo.
Sabha ilikuwa ikichukuliwa miongoni mwa ngome muhimu zilizobaki za majeshi ya Kanali Muammar Gaddafi.
Kuna ripoti za kuwepo na vifo vingi karibu na mji ulio jangwani wa Jufra.
Mmoja aliyeshuhudia aliliambia shirika la habari la AFP kwa simu, "Kulikuwa na watu wengi waliouawa na kujeruhiwa kwenye mji huo na hatuwezi kuwafikia kutokana na mashambulio makali."
Mapigano makali pia yanaendelea katika ngome zengine za Kanali Gaddafi, Bani Waild na Sirte.
0 Comments