Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza mpango wa kubuni kazi utakao gharimu dola bilioni 450.
Katika hotuba ya kipekee mbele ya bunge la Congress, rais Obama amesema mpango huo utasaidia kuuchepua uchumi wa nchi hiyo. Rais Obama ameahidi kubuni nafasi zaidi za kazi katika sekta ya ujenzi, elimu na pia kwa wanajeshi wastaafu na wale ambao hawana kazi, na pia kupunguza kodi.
Spika wa bunge la waakilishi ambaye ni mwanachama wa Republican, John Boehner, amesema mapendekezo ya Obama yatachunguzwa kwa kina na wabunge wa chama chake.
0 Comments