Umoja wa Mataifa umesema Sudan na taifa jipya la Sudan Kusini, yameafikiana kuondoa wanajeshi wao katika eneo linalozozaniwa la Abyei ifikapo mwisho wa mwezi huu.
Naibu mkuu wa jeshi la Umoja wa mataifa la kulinda amani, Edmond Mulet, amesema mkataba huo, umeafikiwa kwa urahisi kwa sababu wanajeshi wa Umoja huo kutoka Ethiopia wanahudumu katika eneo hilo la Abyei.
Mataifa haya mawili yameshindwa kukubaliana kuhusu ni nani anayestahili kudhibiti mji huo suala ambalo limezua mzozo mkali kati yao.
Mwandishi wa BBC nchini Sudan anasema kuwa, uhasama kati ya nchi hizo mbili utapungua kwa kiasi kikubwa kufuatia uamuzi huo.
0 Comments