Rwanda imeshtumu jeshi la Ufaransa kwa kuchangia katika mauaji ya watu 800,000 wengi wao wakiwa kabila la watutsi waliouawa na utawala wa kabila la wahutu na washirika wake.

Uhusiano wa kibalozi ulivunjwa mwaka 2006 baada ya jaji wa kifaransa kumlaumu Bwana Kagame, ambaye wakati wa mauaji ya kimbari alikuwa akiongoza kundi la waasi la watutsi, kwa kuchochea mauaji hayo.

Pande zote mbili zimekanusha madai yaliyotolewa.

Diplomasia


Mchakato wa kurudisha uhusiano ulianza mwaka uliopita wakati Rais Nicolas Sarkozy alipozuru Rwanda.

Wakati huo, Bwana Sarkozy alikiri kuwa Ufaransa ilifanya "makosa" katika kipindi cha mauaji ya kimbari - lakini hakuomba msamaha.

Alisema "hali fulani ya upofu" ilifanya Ufaransa ishindwe kuona "sehemu ya mbinu za mauaji ya kimbari kwa upande wa serikali" wakati huo.