Rais Kikwete ambaye aliondoka usiku wa jana kwenda nchini Marekani, kuhudhuria mkutano huo wa 66 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (Unga), na mikutano mingine ya viongozi wa nchi na Serikali yenye maslahi kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandishi maalum wa Ikulu, imesema Rais atashiriki ufunguzi wa mkutano huo, pia atashiriki mkutano wa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Umoja wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria ( ALMA), ambao yeye ni mwenyekiti.
Mbali na Rais Kikwete waalikwa wengine ni marais Paul Kagema wa Rwanda, Goodluck Jonathan wa Nigeria na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.
Aidha baada ya mikutano hiyo, Rais Kikwete atashiriki katika Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Rais Clinton ya Clinton Global Initiative na atahudhuria mkutano maalum wenye mada ya Putting Teeth into Non-Communicable Disease unaondaliwa kwa pamoja na Tanzania, Australia na Sweden.
Baadaye jioni atakuwa msemaji mkuu katika hafla ya viongozi ya nchi na Serikali kusheherekea mafanikio ya muongo uliopita ya kupambana na ugonjwa wa malaria ulioandaliwa na taasisi ya Roll Back Malaria. Miongoni mwa watakaohudhuria halfa hiyo ni Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk. Asha-Rose Migiro.
Kwa mujibu wa ratiba ya rais nchini humo, kesho atashiriki katika mkutano wa viongozi wa nchi na Serikali kuhusu Lishe na baadaye mchana atajiunga na Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon kushiriki katika hafla ya viongozi iitwayo “Every Woman, Every Child Leaders Event”.
Mchana Rais Kikwete atashiriki katika tukio maalum la kujadili mikakati ya kimataifa kuhusu afya ya wanawake na watoto ya Global Strategy for Women’s and Children’s Health.
Jumatano atakuwa katika ufunguzi wa majadiliano ya mada kuu ya Unga mwaka huu, pia atashiriki katika mjadala kuhusu hali ya chakula wa Beyond Food Security, pamoja na mkutano wa viongozi wa Social Good Summit ambako atapewa tuzo maalum kutoka Umoja wa Mataifa kwa mchango wake mkubwa wa kuimarisha afya ya wanawake na watoto.
Rais Kikwete atahudhuria mikitano hiyo hadi Ijumaa ziara yake itakapomalizika.
CHANZO: NIPASHE (picha kutoka maktaba)
0 Comments