Jamhuri ya Somaliland, ambayo imejitenga na Somalia, imetangaza kuwa wageni wote wanaoishi nchini humo kinyume na sheria lazima waondoke katika muda wa siku 30.
Taarifa iliyotolewa na rais, ilisema mtu yoyote aliyeshindwa kufuata amri hiyo, atashtakiwa na kusafirishwa kwa lazima.
Mwandishi wa BBC anasema, taarifa hiyo itawaathiri wageni kutoka Ethiopia, ambao wanafanya kazi za majumbani, ulinzi, ukulima na ufugaji nchini Somaliland.