Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na MKurugenzi Mtendaji wa PSI Tanzania, Romanus Mtung’e, katika semina ya Wahariri na Waandishi wa habari.
Mtung’e alisema ongezeko la matumizi ya kondomu hapa nchini yanatoa mwelekeo mzuri dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo.
Alisema uelewa kuhusu ugonjwa huo umetokana na ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali pamoja na mshirika yote yaliyopo katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Alitaja mafanikio yaliyopatikana ni kushuka maambukizi mapya kutoka asilimia 7.8 mwaka 2008, hadi kufikia asilimia 5.7 mwaka jana.
Dk. Alex Ngaiza kutoka PSI, alisema wanaume wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wameathirika kwa asilimia 4.6 wakati wanawake wenye miaka kama hiyo ni asilimia 6.6.
Alisema wanawake wajawazito wanaopimwa, asilimia 8.2 wanakutwa wameathirika na kwa nchi nzima hivi sasa watu milioni 1.5 wameambukizwa virusi huku asilimia 10 kati yao wakiwa ni watoto.
0 Comments