Alitoa tahadhari hiyo wakati akizunguma na wananchi wa mjini Mpanda katika mkutano wa hadahara uliofanyika uwanja wa Kashaulili.
Pinda alisema baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakitoa maneno ya kubeza maendeleo yaliyofanywa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema wakati umefika kwa watu wanaoikosoa serikali kwa kila jambo wanayesema mambo mazuri yanayofanywa na serikali iliyopo madarakani.
“Wapo hawa jamaa wanaoshinda vijiweni ambapo kazi yao ukipita wanasema mzee njaa, sasa sijui wanataka uwachukulia chakula mdomoni ukawape, fanyeni kazi,” alisema Pinda na kutaka wakazi wa Mpanda waige mfano wakazi wa kijiji cha Majalila ambao vijana wanajituma kufanya kazi.
Waziri Mkuu alitoa mfano kwamba katika msimu wa kilimo wa mwaka huu yeye alilima hekta kadhaa ambapo amefanikiwa kuvuna magunia 332 ya mahindi ambayo ameyauza na kupata Sh. milioni 11.
Alisema tofauti zilizojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana zimalizwe kwani hayo yameshapita hivyo kinachotakiwa hivi sasa ni watu kushirikiana na kushikamana kwa kufanya kazi ili kujiletea maendeleo na kuahidi kuwa viongozi wa serikali kwa upande wao watahakikisha suala la amani na utulivu linasimamiwa.

0 Comments