NA JOSEPH SHALUWA(risasi Mchanganyiko)
STADI wa muziki wa Bongo Fleva, Mohammed Mbwana ‘MB Dog’ (pichani) amenusurika kuuawa baada ya kufyatuliwa risasi na majambazi jijini Pretoria, Afrika Kusini, Risasi Mchanganyiko lina mkoba wenye data kamili.
Chanzo chetu makini cha habari kinaeleza kuwa MB Dog alipatwa na kadhia hiyo akiwa na rafiki zake watatu akiwemo mjomba wa mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2006, Neema Chande aitwaye Dickson Sekwau na wengine wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja.Sekwau palepale, ambapo baadaye alipata msaada na kufikishwa katika Hospitali ya Steve Bicco Academic iliyopo Pretoria.
“Alikuwa na hali mbaya sana, ilibidi akimbizwe haraka chumba cha upasuaji, akafanyiwa oparesheni, lakini baadaye wakagundua bado alikuwa na tatizo kwenye ubongo, wakarudia tena oparesheni, haikusaidia.
“Alilazwa ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum) hospitalini hapo kwa wiki tatu kabla hajafariki,” kilipasha.
Mwandishi wa habari hizi aliwasiliana na Neema Chande katikati ya wiki iliyopita kwa njia ya Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kumwuliza kuhusu habari hizo ambapo alijibu kwa kifupi: “Ni kweli kaka, nimempoteza mjomba wangu, alikuwa kila kitu kwangu.”
Baadaye alipotakiwa kueleza mazingira ya kifo hicho na taratibu nyingine, alijibu: “Kwa sasa nimechanganyikiwa kabisa, sina cha kusema, lakini fahamu kwamba uncle wangu amefariki, tunafanya mipango ya kusafirisha mwili kuja huko Tanzania.”
Juzi, Jumatatu mwandishi wetu alijaribu kumtafuta Neema kwa njia ya simu na kufanikiwa, ambapo alisema kwamba waliingia Dar Jumamosi usiku wakiwa na mwili wa marehemu.
“Tumekuja juzi (Jumamosi) usiku, jana (Jumapili) tumemzika mjomba, nina huzuni sana maana alikuwa msaada mkubwa kwangu. Ndiye aliyekuwa akinisaidia kila kitu katika masomo yangu,” alisema.
Risasi Mchanganyiko: Pole sana Neema, vipi hali ya MB Dog?
Neema: Yeye ni mzima, unajua kwa bahati nzuri alifanikiwa kukimbia, hajaumia. Mungu alimsimamia.
Risasi Mchanganyiko: Naye amekuja Bongo?
Neema: Ndiyo, tulikuja naye.
Jitihada za kumpata MB Dog azungumzie tukio hilo hazikuzaa matunda, baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana muda wote aliopigiwa.
Habari zinasema kuwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea Septemba 28, mwaka huu, wakiwa njiani kutokea Victoria kuelekea Pretoria, nchini humo.
Inaelezwa kuwa wakiwa njiani, ghafla gari lao lilizingirwa na majambazi ambao walianza kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatisha.
“Walikuwa wanne; MB Dog, mjomba wake Neema (Sekwau) na wengine wawili, wakatekwa na majambazi. Inavyoonekana walikuwa na nia ya kuiba gari... Mb Dog na wenzake walifanikiwa kukimbia na kunusurika, lakini kwa bahati mbaya mjomba wake Neema alipigwa sana.
“Walikuwa wanampiga kwa mtindo wa kumtikisa na kumwangusha chini kisha kumkanyaga kichwani kwenye lami. Aliumia sana kichwani, damu ilivujia kwenye ubongo,” kilieleza chanzo chetu.
Hata hivyo, habari zinasema kuwa majambazi hao hawakufanikiwa kuiba gari la Sekwau kwa vile mmoja wa waliokimbia aliondoka na ufunguo.
Taarifa zinaendelea kupasha kuwa baada ya majambazi kushindwa jaribio la kuiba gari, walikimbia na kumuacha
0 Comments