Marekani imeanza kufanyia majaribio ndege zake za kivita zisizo na rubani nchini Ethiopia katika maandalizi ya kuanza mashambulio dhidi ya ngome za wapiganaji wa Al Shabaab katika nchi jirani ya Somalia.
Ndege hizo ambazo zinaweza kubeba makombora na mabomu yanayoelekezwa kwa kutumia mtambo wa satelite zitaruka kutoka kituo cha jeshi la Marekani katika mji wa kusini mwa Ethiopia wa Arba Minch.
Marekani hata hivyo imeihakikishia serikali ya Ethiopia kwamba ndege hizo hazina silaha kwa hivi sasa na zinatumika tu kuchunguza hali ya usalama.
Marekani imekuwa ikitumia ndege hizi nchini Djibouti ambako majeshi yake yana ngome yake ya kudumu ya kipekee barani Afrika.
0 Comments