Polisi wakitumia helikopta na magari wanawasaka watu watu wenye silaha waliowateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya.
Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika.
Dereva wao, raia wa Kenya, alijeruhiwa na sasa amepelekwa hospitali, limesema shirika la MSF.
Katika wiki za hivi karibuni, wanawake wawili, mmoja raia wa Uingereza na mwingine Mfaransa walitekwa karibu na mpaka huo.(pichan juu ni kambi ya daadab nchin Kenya).
0 Comments