Shughuli ya kupiga kura inaendelea nchini Morocco ambapo raia wanawachagua wabunge wapya.
Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu kuidhinishwa katiba mpya ya mageuzi iliyopendekezwa na mfalme Mohammed wakati nchi za kiarabu zikishuhudia maandamano ya kiraia kushinikiza mageuzi ya kisiasa.
Katiba mpya iliyopendekezwa na mfalme Mohamed inatoa mamlaka zaidi kwa bunge na Waziri Mkuu.
Mfalme sasa anatakiwa amteue Waziri Mkuu kutoka chama kitakachokuwa na viti vingi bungeni badala ya kumteua anayemtaka kama ilivyokuwa hapo awali.
Kinyang'anyiro cha uchaguzi kinaonekana ni kati ya chama cha upinzani cha Kiislamu kinachozingatia msimamo ya kadri wa kidini na mseto mpya wa vyama uliokurubiana sana na mfalme.
Chini ya katiba mpya, mfalme ndiye atakayekuwa na mamlaka ya kipekee ya kutoa maagizo katika masuala ya ulinzi, usalama na dini .
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa mbili asubihi na vitafungwa saa moja za usiku saa za Morroco. Raia milioni 13.5 wa Morrocco wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua wabunge katika viti 395.
0 Comments