Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 28, 2011

MIMBA YA WEMA SEPETU YATOKA

HUJAFA hujaumbika! Ni habari mbaya inayogusa ‘kapo’ ya Wema Isaac Sepetu na Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ baada ya mnyange huyo kupoteza uzao wao kufuatia mimba yake ya takribani miezi miwili kuchoropoka, Ijumaa Wikienda linairusha hewani ‘laivu’ bila chenga.

TUJIKUMBUSHE SIKU YA FURAHA
Wiki kadhaa zilizopita, huku akiwa na furaha, Wema ambaye ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo, alisimama mbele ya kamera za video za gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko na kuthibitisha kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu baada ya kutoka kwenye vipimo (pregnancy test).

“Ni jambo la furaha sana, ni muda muafaka kwangu kupata mtoto,” alinukuliwa Wema akiwa hachezi mbali na ubuyu, ndimu na maembe mabichi.

CHANZO
Wiki mbili baadaye, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake na mazungumzo yalikuwa hivi;
Chanzo: Ijumaa Wikienda mna habari?

Wikienda: Habari tunazo nyingi tu, soma magazeti ya Global Publishers, lakini kama una ya kwako, nayo ni muhimu ukitupatia tutairusha hewani.

Chanzo: Kwa taarifa yenu, mimba ya Wema imechoropoka na hapa tunapozungumza yupo hoi kitandani, anaumwa.
Wikienda: Una uhakika? Amelazwa hospitali gani?

Chanzo: Kwani nilishawahi kuwadanganya? Yupo nyumbani anakoishi na Diamond, Sinza-Madukani, Dar. Sitaki mahojiano zaidi, fuatilieni mtajua ukweli na tafadhali naomba msinitaje.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya maelezo hayo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni na kujikusanyia data zilizokaribia kwenye ukweli kutoka kwa watu wa karibu na wapenzi hao.

Hata hivyo, timu ya Ijumaa Wikienda ilipotaka kumuweka Wema kwenye ‘tageti’, alisafiri na Diamond kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya shoo na mapumziko mafupi.AREJEA BONGO, AWEKWA ‘MTUKATI’ Aliporejea Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa Wikienda lilimuweka ‘mtukati’ na kumtaka kuonesha kibendi kilipoyeyukia. Alifunguka huku akijua kuwa akibisha, aibu itamfika kwani hana tena kile kitumbo kilichogeuka kero kwa mastaa wenzake kufuatia kutema mate ovyo.
Alisema: “Ilikuwa Jumatatu ileee (wiki mbili zilizopita), nilikuwa katika hali mbaya na baadaye niligundua kuwa mimba yangu inachoropoka. Nilikimbilia ‘famasi’ ya Primar na kumweleza mtaalamu hali yangu.
“Aliniambia mimba yangu imechoropoka hivyo nilipatiwa dawa kwa ajili ya kusafisha kizazi.

MUNGU HAKUPANGA AZAE?
“Ukweli niliumia sana, lakini nilijua Mungu hakupanga nizae wakati huu, najua amenipangia muda muafaka.
“Nahisi chanzo ni vipigo vya ‘toto yangu’ (Diamond Platinum Baby), lakini pia nahisi ni kwa sababu ya matumizi ya pombe kali.

DIAMOND ALIA KAMA MTOTO MDOGO
“Nilipomjulisha Diamond juu ya kupoteza kiumbe chake tumboni, alijisikia vibaya sana, alilia kwa uchungu kama mtoto mdogo.
“Kwa sasa niko fiti kabisa na namuomba Mungu nishike ujauzito mwingine kwani natamani kupata mtoto kuliko kitu kingine chochote.”

DIAMOND VIPI?
Diamond alikiri kumtandika Wema kutokana na kushindwa kuzuia hasira hasa mwanadada huyo anapomkosea, lakini hakuweza kuzungumzia kuchoropoka kwa ujauzito huo.
“Hata makofi muda mwingine yanafunza,” alisema Diamond.


ATHARI YA VIPIGO NA
POMBE KALI KWA MJAMZITO
Diamond na wanaume wengine wanapaswa kujua kuwa kasumba ya mwanaume kumpiga mwanamke ni ya kizamani na mke hapigwi makofi bali kwa upande wa khanga.

Pia Wema na wanawake wengine wanatakiwa kujua kuwa kunywa pombe wakati wa ujauzito ni sawa na kumpiga mwanao nyundo akiwa hai na kumuua.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP