NI AIBU! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Salama Hamza ambaye anadaiwa kuwa ni mke wa mtu amezua tafrani baada ya kunaswa laivu katika maeneo ya wadada wanaofanya biashara ya kukodisha miili almaarufu machangudoa, Amani lina mkanda mzima.
Inaelezwa kuwa, Salama ni mke halali wa Hamduni Omar ambaye anaingiza siku kwa kufanya kazi ya ulinzi katika kampuni moja jijini Dar es Salaam, yenye makao yake Ilala na kwamba wawili hao wameweka makazi yao Tandika.
Mtiti mzima ulichukua nafasi Jumatatu ya wiki hii, saa tatu na dakika zake asubuhi, pande za Kinondoni ambapo ilielezwa kuwa Salama alikuwa akiuza ‘sukari’ usiku wa kuamkia siku hiyo, lakini kwa bahati mbaya alilewa na ‘kuzima’ hadi alipozinduka asubuhi hiyo na kufumwa na shemeji yake.
CHANZO KINAMIMINIKA
Amani likiwa ofisini likiendelea kutimiza majukumu yake ya kila siku, simu iliita na ilipopokelewa ilikutana na sauti ya kiume iliyotoa ‘tipu’ ya stori hiyo.
“Kuna vurugu huku Kinondoni Kwamanyanya, njooni mchukue habari. Mke wa mtu amefumwa na shemeji yake, yaani ni changudoa kabisa anayejiuza hapa kila siku,” alisema mtoa habari huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini.
Kama kawa, kama dawa, kazi ya gazeti hili ni kufuatilia matukio na kuyaandika, hivyo bila kupoteza muda, kikosi kazi kiliingia mtaani kama ‘maninja’ ili kujionea.
MAMBO, MAMBO WAAA...
Waandishi wa Amani walipofika eneo hilo, walikuta kimbembe hicho kikiwa bado ‘hot’ kabisa ambapo Salama alikuwa akikimbizana na mwanaume mmoja aliyetajwa kuwa ni shemeji yake.Kutokana na utulivu kuwa sifuri, mapaparazi wetu waliamua kuanza na zoezi la kupiga picha kwanza kabla ya kupata maelezo kutoka kwa pande zote (angalia picha ukurasa wa mbele).
SHEMEJI MTU ALALAMA
Wakati purukushani kati ya Salama na shemeji yake zikiendelea, jamaa huyo alisikika akimlaumu kwa kitendo cha kumsaliti kaka yake kwa vile anafanya kazi ya ulinzi usiku.
Kwa uchungu, kijana huyo alimwambia Salama: “Yaani kuhudumiwa kote na kaka hutosheki, kweli nimeamini kunguru hafugiki. Kwa usalama wako simama turudi nyumbani. Sitakubali kabisa kwa kitendo hiki unachomfanyia ndugu yangu.”
Baada ya kuonekana kunaweza kutokea hali ya hatari, mashuhuda waliamua kumshika Salama na wengine wakamsihi jamaa atulize jazba kwa kuwa ni mambo yanayoweza kumalizika kifamilia.
Akizungumza na gazeti hili, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dulla alisema: “Ndugu zangu, sina haja ya kujipendekeza, huyu ni shemeji yangu kabisa. Ameolewa na kaka yangu wa damu ambaye anafanya kazi ya ulinzi. Nimeshtuka sana kumuona hapa muda huu, tena akiwa hivi (nusu utupu).“Salama huwa havai nguo za namna hii? Nimezoea kumuona na khanga mbili au baibui tu; sasa hapa hamuoni kaka yangu anaonewa? Anatumia vibaya nafasi anayoipata wakati kaka akiwa kazini, sikubali. Hawezi kumuua ndugu yangu.”
MASHUHUDA WATIA NENO
“Huyu dada ana kawaida ya kuja maeneo haya na machangudoa wenzake kila siku usiku, ila huwa anaondoka kati ya saa 10 na 11 alfajiri, lakini jana alipotoka kwa babu (akimaanisha kwa mlinzi anayetoa huduma ya sehemu ya kufanyia ngono chapchap) alifika hapa na kuagiza kiroba.
“Alipomaliza akaongeza kingine, halafu zikafuata bia. Alikunywa sana hadi akalala kwenye kiti. Alipoamshwa hakusikia. Sasa asubuhi hii huyu jamaa alifika hapa na kuagiza supu ya utumbo, nikaona anamkazia macho kabla hajamvaa.
0 Comments