Bwana Laila Odinga akishuka toka kwenye ndege,pindi alipowasili nchini Tanzania.
Akisalimiana na mwenyeji wake ambaye ni mmiliki wa Quality Centre, Yusuf Manji. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq.
WAZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, jana jioni alitua hapa nchini kwa ajili ya shughuli za uzinduzi wa jengo la kisasa la biashara la Quality Centre, lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. Shughuli hizo hizo zinatarajiwa kuzinduliwa leo asubuhi.