Rais wa Marekani Barack Obama ameadhimisha kumalizika kwa vita vya Iraq kwa kupongeza "mafanikio yasiyo ya kawaida" kwa vikosi vya Marekani katika mapigano ambayo yalipingwa sana.
Katika hotuba kwenye eneo la Fort Bragg huko Carolina Kaskazini, aliwapongeza wanajeshi wale waliodumu na kufariki dunia wakiwa vitani, pamoja na jamii zao.Wanajeshi wa Marekani wa mwisho wanatarajiwa kuondoka kabisa Iraq katika siku chache zijazo.
Wajumbe wa chama cha Republican wamekosoa mpango huo wa kuondoa wanajeshi wakielezea wasiwasi kuhusu usalama wa Iraq, lakini raia wengi wa Marekani wanaunga mkono hatau hiyo.
Katika hotuba ya Jumatano, Rais Obama - ambaye kwa kiasi fulani alifanikiwa kuwa rais kwa msimamo wake wa kupinga vita vya Iraq - alipongeza ujasiri wa majeshi ya Marekani katika muda wa miaka takriban tisa kweney vita hivyo.
0 Comments