Kifo cha Ngahyoma aliyekuwa mtangazaji na mwandishi wa shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Tanzania akiripoti kutoka Dar es Salaam na viunga vyake kimekuja siku moja baada ya mtangazaji mwingine mkongwe wa kike aliyejizolea sifa kubwa ya utangazaji mpira Haklima Mchuka kufariii ghafla huku mipango ya maziko yake ikiendelea.
Ngahyoma aliyewahi kufanya kazi katika vituo vya taifa vya redio cha Redio Tanzania Dar es Salaam na baade kujiunga na IPP Media katika vituo vya Redio One na ITV ambako pia aliondoka na kujiunga na BBC ameripotiwa kufariki hii leo jijini Dar es Salaam.
Tasnia ya habari nchini Tanzania kwa kipindi cha siku mbili itakuwa imeapatwa na pigo kubwa kufuatia vifo vya waanahabari hao wawili wa siku nyingi.
Marehenu Ngahyoma amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu na hata kwenda nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia maradhi yaliyokuwa yakimsibu.
Taarifa ya haraka iliyotumwa katika mitandao ya kijamii (blogs) na Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri (TEF) Neville Meena inasema msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea jijini Dar es Salaam jirani na kwa Mwandishi mwingine aliyefariki miezi kadhaa iliyopita Danny Mwakiteleko.
Aidha Meena ameomba mtu yeyote atakaekuwa na taarifa zaidi kuhusiana na mipango ya maazishi ya Marehemu Ngahyoma kumfikishia.
0 Comments