Luqman Maloto na Vyanzo Mbalimbali
 TANZANIA inatahadharishwa, inaonywa kuhusu mkakati wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemasons kwamba inamuandaa rais wa tano, atakayeingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kutokana na onyo hilo, hofu inatanda kwa wananchi wenye imani za kidini hususan Waislam na Wakristo kwamba baada ya Rais Jakaya Kikwete, kiongozi ajaye anaweza kuwa mfuasi au kibaraka wa Freemasons.

Kwa sehemu kubwa, Freemasons inatajwa kuwa ni Dini ya Shetani kutokana na kile kinachodaiwa kwamba wafuasi wake wengi humuabudu Shetani (Jini Mkuu), Lucifer.

Kuhusu mtindo ambao Freemasons watautumia kusimika rais wao 2015, Watanzania wanaonywa kuhusu mwanasiasa ambaye atang’ara kwa kasi ya kutisha ndani ya kipindi hiki kuelekea mwaka 2015.

Mtaalamu wa mambo ya Freemasons, Maalim Hassan Yahya Hussein, aliliambia Uwazi kuwa Waislam na Wakristo wanatakiwa kudumisha maombi, vinginevyo jamii hiyo ya siri itakita mizizi yake nchini na hatimaye kusimika kiongozi mkuu wa nchi wanayemtaka.

Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za aliyekuwa Mnajimu Maarufu Afrika, marehemu Sheikh Yahya Hussein, alisema kuwa vita ya Freemasons kwa sasa ni kuhakikisha wanatimiza azma yao ya kuitawala dunia kabla ya ujio wa Yesu ambaye yumo ndani ya imani za Kikristo na Kiislam ambayo humtambua kwa jina la Nabii Isa.

Alisema, Freemasons wapo kwenye mapambano ya muda ili kumuwahi Yesu kwa kuhakikisha inashika nyanja za utawala ndani ya kila nchi, kwa kuweka marais, maspika wa bunge na majaji wakuu ili kurahisisha njama za kwenda kwenye dunia yenye serikali moja, itakayoamini dini moja (Dini ya Shetani).

“Ni mpango wa Shetani, maandiko yanaeleza kuwa Shetani alimuahidi Mungu kwamba atahakikisha binadamu hawamfuati Mungu na wanakwenda kwake, ndiyo maana ya kuwepo kwa harakati hizi.
“Freemasons wanataka dunia iwe inaabudu Dini ya Shetani, dunia nzima iwe na serikali moja, itumie sarafu moja na ili mtu apate huduma ya kijamii, itabidi awe mfuasi wao na atatambulika kwa namba ambazo watu watachapishwa kwenye miili yao,” alisema Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa marehemu Sheikh Yahya.



Kuhusu jinsi Freemasons wanavyoweza kupenya nchini na kuweka rais wao, Maalim alisema: “Kwanza wapo hapa Tanzania, tena wapo bize sana kufanya mapinduzi wanayoyataka. Kila siku wanajaribu kufikia mihimili yenye nguvu.

“Wanahakikisha wafanyabiashara wakubwa wote wanakuwa wafuasi wao, wale wanaogoma kuwafuata, wanafanya juu chini ili kuwafilisi. Freemasons wapo ndani ya Tanzania.”
 Maalim alisema kuwa mtindo ambao Freemasons wanautumia ni kumtumia kiongozi ambaye tayari anaonekana kuwa na mvuto kwenye jamii, hivyo kumpaisha zaidi na kuhakikisha inavunja vikwazo vyote vinavyoweza kufanya asiwe rais.

Alitoa mfano kwamba katika sura ya siasa ya Tanzania, wanasiasa ambao wanaweza kuwindwa na Freemasons kutokana na mvuto wao wa kisiasa ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni aliye pia Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

Ndani ya Chadema, mwingine anayeweza kuwindwa na Freemasons kutokana na mvuto wake ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, aliye pia Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu.

Katika CCM, aliwataja wanasiasa wenye nguvu kuwa ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-rose Migiro, Katibu Mkuu wa zamani wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) sasa Umoja wa Afrika (AU), Dk. Salim Ahmed Salim, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, William Lukuvi na wengine wachache wanaokubalika.

Imeelezwa kuwa mpaka kufikia nusu ya muhula wa mwaka 2010-2015, tayari Freemasons itakuwa imeshakamilisha uteuzi na yule watakayemtaka watamkabidhi misingi yao na muongozo wa masuala ya kutekeleza akishaingia Ikulu.

Maalim alisema kuwa inawezekana miongoni mwa wanasiasa waliotajwa, hakuna hata mmoja mwenye wazo la Freemasons na wala hajafuatwa lakini muda ukiwadia, atawekwa kitako na kuambiwa yeye ndiye mteule, hivyo kupewa misingi ya imani zao.

Hata hivyo, Maalim alisema kuwa Freemasons hawafungamani na watu wenye imani kali za kidini, mathalan Uislam na Ukristo, akaeleza kuwa wenye misimamo ya wastani na dhaifu ndiyo hupewa kipaumbele.

VITA YA IMANI
Maandiko yanasema kuwa nyakati za mwisho kutakuwa na tishio la dunia kutawaliwa na Dini ya Shetani ambapo zama hizo zikifika kutakuwa na mfumo utakaozuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.

Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya Freemasons ambao taarifa na uchambuzi wao unapatikana kwenye mitandao ya intaneti, jamii hiyo ya siri ndiyo inayotumia chapa 666 na kwa sasa tayari imekwishaanza kutumika, japo wengi hawajui.
Wanasema kuwa chapa hiyo, inapatikana kwenye bidhaa mbalimbali ambazo zinauzwa na kununuliwa karibu nchi zote duniani, huku watu wengi wakitumia pasipo kujua.

Wameeleza kuwa kilichobaki sasa ni mfumo wa kuwalazimisha watu wote duniani kuelekea kwenye imani hiyo ili wapigwe chapa 666 kisha wale watakaogoma, wawe wanakosa huduma muhimu za kijamii.

Inabainishwa kuwa ingawa Jamii za Siri (Dini za Shetani) zipo tatu, zinazojulikana duniani, ikiwemo Illuminati na Skull & Bones, Freemasons ndiyo yenye nguvu na imeshawasimika viongozi wa mataifa yenye nguvu duniani.